GET /api/v0.1/hansard/entries/757531/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 757531,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/757531/?format=api",
    "text_counter": 85,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Limo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1915,
        "legal_name": "Joseph Kirui Limo",
        "slug": "joseph-kirui-limo"
    },
    "content": "Kwa hivyo, tunataka kupiga kura na wananchi wote wanajua ni nani watampigia kura na wanajua ni nani walimpigia. Korti haikusema Uhuru Kenyatta hakushinda. Hakuna siku hata moja mahakama ilisema hivyo. Walisema karatasi fulani haikuwa imewekwa nambari fulani. Juzi tumesikia kuwa hizo karatasi zote zilikuwa sawa. Turudi kwa uchaguzi. Mambo ya mkate nusu hakuna. Hatuwezi kujifanya kwamba jamaa huyu anataka mkate nusu. Nataka kuwaambia wale wanaotembea na Raila Odinga; Mudavadi na Kalonzo, wajitayarishe. Raila Odinga aliitisha maandamano halafu baada ya siku moja, akasema hakuyaitisha. Anataka kwenda kando ndiyo wengine waingie shimoni wapelekwe Hague. Yeye ndiye atapelekwa Hague. Hawezi kupeleka mtu mwingine kama alivyompeleka William Ruto. Tunajua hayo na lazima tuseme. Tutafanya uchaguzi tarehe 26 mwezi wa kumi. Ahsante, Mhe. Spika."
}