GET /api/v0.1/hansard/entries/758544/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 758544,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/758544/?format=api",
"text_counter": 182,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1179,
"legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
"slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
},
"content": "huna hekima, yote ni bure kabisa. Hakuna kitu hapo! Sisi tumechaguliwa kuja hapa kutengeneza sheria. Kama wakili angekuwa hapa, ningemwambia ile sheria walitumia kortini ilitengenezwa hapa hapa katika Bunge hili. Kwa hivyo sisi tuna jukumu la kutengeneza sheria. Ninashangaa tunapingana eti muda wa kuchapisha Miswada hii upunguzwe. Ninashituka kama kweli tumechaguliwa na watu. Ni kama nyumba inachomeka lakini tunawaambia wazimamoto wasimamishe kazi yao ya kuzima moto, ili tujadiliane. Hiyo si hekima. Saa hizi tunajua nchi iko na shida na shida ni sisi Wabunge. Kwa hivyo, ningewaomba wenzangu tujadiliane ili tupoeshe moto unaowaka nchini. Kura ilipigwa na korti haikusema eti Rais hakushinda. Tunalozungumzia ni usambazaji wa matokeo. Usambazaji wa matokea ndiyo gari lililobeba matokeo ya kura kutoka huko mashinani hadi Nairobi. Ningependa kuuliza wenzangu walio katika muungano wa NASA: je, tungeleta matokeo hayo kwa wheelbarrow, punda ama pikipiki? Hilo ndilo swali na jibu lake litasaidia nchi ili tuendelee na biashara."
}