GET /api/v0.1/hansard/entries/758926/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 758926,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/758926/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kanini Kega",
    "speaker_title": "The Member for Kieni",
    "speaker": {
        "id": 1813,
        "legal_name": "James Mathenge Kanini Kega",
        "slug": "james-mathenge-kanini-kega"
    },
    "content": " Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nichangie mjadala ambao uko mbele yetu, ambao ni kuangazia kalenda ya muhula huu. Kabla sijachangia, naomba unikubalie kwanza nikupe heko kwa kuchaguliwa katika muhula wa pili na pia kuchaguliwa katika kamati itakayosimamia vikao vyetu. Nilikuwa nataka kuchangia Hoja ambayo ilikuwa hapo mbele, ambapo tulikuwa tunaangazia wale ambao wataketi katika kamati hiyo. Pia, niseme kwamba wote ambao wamechaguliwa, ninawajua. Ni watu ambao wako na tajriba ya hali ya juu, uzoefu na watatupeleka mbele katika mijadala yote ambayo tutakuwa tukichangia hapa. Hii ni nafasi yangu ya kwanza kuongea katika Bunge la Kumi na Mbili. Mimi ni kati ya wale wachache ambao walipata nafasi kuchaguliwa kwa muhula wa pili katika kanda ninayotoka. Kutoka kaunti yangu, Kirinyaga na Laikipia ambazo zinapakana, ni mimi tu niliyeponea. Kwa hivyo, ni shukrani kwa Mungu. Nawashukuru wapiga kura kule kwangu Kieni kwa sababu walinipatia nafasi ya pili kuwahudumia. Wale ambao wamechaguliwa kwa mara ya kwanza, ama muhula huu, ni jukumu kubwa ambalo liko mbele yenu. Nawapa heko. Lakini mujue kwamba kuna wengine ambao walikuwa wamekalia hivyo viti ambavyo mnavikalia sasa hivi. Mhe. Naibu Spika wa Muda, heko pia kwa wale ambao wamechaguliwa kwa muhula wa pili na wa tatu. Wananchi ambao waliwachagua waliona kuna kitu kizuri ambacho kiko hapo. Waswahili husema mvumilivu hula mbivu. Naibu Spika, Mhe. Cheboi alikuwa hapo akiketi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}