GET /api/v0.1/hansard/entries/758927/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 758927,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/758927/?format=api",
"text_counter": 180,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kanini Kega",
"speaker_title": "The Member for Kieni",
"speaker": {
"id": 1813,
"legal_name": "James Mathenge Kanini Kega",
"slug": "james-mathenge-kanini-kega"
},
"content": "katika kiti ambacho umekalia na kwa sasa hivi, yeye ndiye Naibu Spika. Hata mimi naona siku moja, kwa majaaliwa, utakuwa Spika wa Bunge hili. Pili, muhula uliopita nilisema kwamba muhula huu nitajaribu sana niwe nikiongea katika lugha ya Kiswahili, lugha tunayoienzi. Wakati mwingine nikiangalia ama nikitazama mijadala kwenye Bunge la marafiki wetu wa Tanzania, mara nyingi wanatupa changamoto. Kwa nini sisi pia tusiwe na siku kando ambayo ni ya kujadili kwa lugha inayoeleweka na wananchi wale waliotupa kura? Wengi wetu hapa walipokuwa wakiomba kura walitumia lugha ya Kiswahili na ya mama. Ni wachache sana kwa wale wamechaguliwa katika Bunge hili waliokuwa wanatumia lugha ya Kingereza. Naibu Spika wa Muda, kwa mjadala ulioko mbele yetu, ni vizuri tuseme kwamba safari ya kesho hupangwa leo. Kwa hivyo, ni vizuri kuweka mikakati na mipangilio ya kalenda yetu ambayo inatuonyesha zile siku tutakayzofanya kazi hapa kama Wabunge, lakini tujue kwamba kuna ile inaandikwa recess . Recess sio likizo ilhali ni wakati ambao unarudi kule mashinani kuongea na wananchi wako, kuwasikiza wakuambie ni shida gani wanazotaka uwatatulie ndiposa uweze kupata nafasi nyingine ya kuchaguliwa kama Mhe. Kanini Kega. Ni vizuri sana Wabunge wapya wajue kwamba sio kuja tu hapa Bungeni na kuleta Miswada, kuhudhuria mikutano ya hadhara huku wakitoa matamshi ya kuzusha au kutoa rabsha katika taifa hili. Ni vizuri wajue ya kwamba matamshi unayotoa ukiwa kiongozi ndiyo itafanya uonekane kama umekomaa au la. Mhe. Olago Oluoch wa Kisumu Magharibi amesema vizuri sana. Sisi kama Bunge la Taifa tunaangaliwa kote duniani tunapotoa rabsha, malumbano na kutusi wengini ambapo tunachekelewa. Mimi ningewaomba Wabunge wenzangu hasa wa mrengo ule mwingine na hata pia wa mrengo wetu watulize boli maana uwanja ni mdogo. Mambo ya matusi na kuzua rabsha hatutaki. Mhe. Olago Oluoch amesema vizuri kuwa tutatumia likizo hii ambayo tumepewa na Bunge kuenda kuongea na wenzetu maana lazima tutoe mwelekeo. Kuna uchaguzi unakuja tarehe 26 mwezi Oktoba na ni lazima ufanyike kwa amani maanake taifa letu linaenziwa katika kanda hii. Kila mtu anataka kuja Kenya lakini tukianza kuongea mambo mengine ambayo hayaleti ladha nzuri katika taifa letu la Kenya, tutakuwa tukijikosea. Mhe.Naibu Spika wa Muda, sitaki kupitisha hapo. Nataka tu kukutakia kila la heri na kuwatakia Wabunge wote ambao wamechaguliwa kila la heri na niombe sana kwamba tunapofanya mikutano ya hadhara na kuongea na wakubwa wetu, tuhubiri amani maanake viongozi huja lakini Kenya itadumu kama taifa. Tuko na taifa moja ambalo linaitwa Kenya na hakuna mataifa mawili. Kwa hayo machache, asante sana kwa kunipa nafasi hii. Tutashirikiana sana kwa Miswada hapa na pia tukienda kule nje tutakuwa tukihubiri Amani."
}