GET /api/v0.1/hansard/entries/758948/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 758948,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/758948/?format=api",
    "text_counter": 201,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13398,
        "legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
        "slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kabla sijazungumzia kalenda ya Bunge, ningependa kuchangia Hoja iliyokuwa ikizungumziwa hapo awali kuhusu Kenya na ukenya ndani yetu. Naweza kuwa mchanga au mdogo katika Bunge hili kisiasa lakini jana nilipokuwa nimeketi na kujituliza, nilisikiliza Hoja za Wabunge mbalimbali wakijadili masuala ya taifa hili. Kutathmini tu kwa ufupi, niliona kwamba katika Bunge hili hapo jana, mada ilikuwa ni Raila-Uhuru, NASA-Jubilee na tutunge sheria-tusitunge sheria. Watu wengi pia walijaribu kuzungumzia mifano mbalimbali na kufanya nchi mbalimbali kama mifano, ikiwemo Ujerimani, huku wakilitaka taifa hili lisonge mbele kisheria ambayo labda sheria yenyewe imependekezwa na vile mtu binafsi anavyoiona. Kwa ufupi, mimi nasema kwamba iwapo hatutakuwa waangalifu kama viongozi, taifa hili litakwenda katika hali mbaya sana. Mwaka wa 2007, baada ya uchaguzi, nchi hii ilitumbukia katika ghasia za baada ya uchaguzi. Tunachoona sasa ni dalili ya mambo mengine mabaya kuzidi kushamiri. Waswahili wanasema kwamba mimba ya mwanaharamu huingia mara ya kwanza. Ya pili ni kusudi. Mimba ya Kenya iliingia mwaka wa 2007 wakati ambapo tuliwapoteza watu zaidi ya 1,000 na jinsi ambavyo tunajadili katika Bunge hili, huenda kukachangia zaidi maana watu wengi wanajadili kwa misingi ya chama, kabila, dini na chaguo la kiongozi wanayemtaka."
}