GET /api/v0.1/hansard/entries/758957/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 758957,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/758957/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13398,
        "legal_name": "Amin Deddy Mohamed Ali",
        "slug": "amin-deddy-mohamed-ali"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Kwa ufupi, nilikuwa nasema tujaribu kutunga sheria katika Bunge hili. Tutunge sheria ya Kenya na ukenya ndani yetu. Tusitunge sheria kwa sababu ya vyama kwa sababu taifa hili likizama, tutazama sote. Sisi kuwa katika Bunge hili nadhani tumekuja hapa sote kwa ajili ya suluhu na suluhu hii ni kwa taifa zima, sio kwa Wabunge peke yake. Kwa hivyo, lolote lile ambalo tutakuwa tukifanya katika Bunge hili, basi liwe ni katika misingi ya kuhakikisha kwamba taifa hili linasonga mbele. Mambo yote ambayo yanatokea kuhusiana na jinsi ambavyo Wabunge wanazungumza katika mikutano ya hadhara yanatokana na sisi kuonyeshana ubabe wa vyama. Sisi kama wagombea huru nadhani tuna nafasi nzuri kwa sababu hatumulikwi na mtu yeyote yule, bali tunamulikwa na watu waliotuchagua na kutuleta katika hili Bunge."
}