GET /api/v0.1/hansard/entries/759190/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 759190,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/759190/?format=api",
"text_counter": 136,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja hii. Waliochaguliwa kuhudumu katika hili jopo ni Maseneta walio na umaarufu na uzoefu wa kazi. Sen. Fatuma Adan Dullo, Sen. Wamatangi, Sen. Sakaja, Sen. Naomi na Sen. Cheruiyot wana uzoefu na kwa hivyo itawezekana. Pili, kazi ya Bunge ni kutunga sheria. Hakuna wakati utakaosemwa ni mzuri au mbaya. Wakati wowote ni wa kutunga sheria. Hiyo ndiyo kazi yetu. Kazi yetu ni kutunga sheria. Huwezi ukasema wakati fulani ni mzuri wa kutunga sheria. Sheria yoyote ambayo inaonekana kuwa na upungufu inapaswa kutengenezwa wakati unaofaa. Hii inatupa fursa njema, hasa kwa wale wanaonung’unika ya kwamba kulikuwa na shida wakati wa uchaguzi. Wanaweza kuja wakaliona hili jopo wakaleta malalamishi yao yote hapa badala ya kwenda kwa maandamano huko nje. Hii ni kwa sababu hata wakiandamana huko nje sheria inatengenezwa katika Bunge. Jambo lingine nzuri ni kuwa kukiwa na upungufu katika sheria, ikiletwa Bungeni itaangaliwa vizuri zaidi kwa maana isipoangaliwa vizuri zaidi, ikipelekwa kwa Korti, wale Mahakimu watafanya vile watakavyofanya – I mean they can legislate from thebench if there is ambiguity ---"
}