GET /api/v0.1/hansard/entries/759260/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 759260,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/759260/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "tulikuwa na kura ya mlolongo ambapo wale waliokuwa na milolongo mifupi walichaguliwa kama viongozi na wale waliokuwa na milolongo mirefu walinyimwa uongozi. Hapo ndipo vuguvugu la kubatilisha sheria za uchaguzi na katiba zilianza humu nchini. Kwa muda wote huo, Wakenya wengi walijitahidi na wengine walipoteza Maisha yao kwa sababu walikuwa wanataka kuwe na uchaguzi wa haki na usawa nchini. Kwa hivyo, iwapo tutajadili na kupitisha sheria hii, tutairejesha nchi yetu katika muhula wa fujo, ghasia na mambo mengine kama hayo ambayo si mazuri kwa nchi yetu ya Kenya. Katika uchaguzi uliopita, ningependa kuwapongeza Jaji Mkuu Maraga na majaji wenzake kwa uamuzi wa busara waliofanya. Mahakama Kuu, Supreme Court, ilionyesha ujasiri kwa kudhibitisha ya kwamba nchi ya Kenya ina katiba na sheria za kuendesha mambo yake. Hii ilikuwa ni ujumbe kuwa nchini Kenya lazima tufuate mambo kwa mujibu wa sheria. Kwa hivyo, hatuwezi sasa kuamka na kujaribu kubatilisha sheria za uchaguzi wakati siku ya uchaguzi, tarehe 26 Oktoba, 2017 inapowadia. Hatuwezi kubatilisha sheria za mchezo wakati mchezo unapoendelea. Hilo ni wazi na hakuna atakaye likubali. Vile vile, ilionekana kuwa tatizo si kwamba sheria ni mbaya bali ni wanaotekeleza sheria. Kuna mvutano katika IEBC kati ya makamishna wenyewe na baina ya makamishna na wafanyikazi kama Bw. Chiloba. Kwa hivyo, matatizo hayo yanahitaji kutatuliwa na sio sheria ambazo zilizoko. Sheria ni msumeno, inakata mbele na nyuma. Kwa hivyo, swala la kubadilisha sheria za uchaguzi kwa sasa ni swala ambalo halifai kwa sababu tayari kuna mvutano nchini. Kuna baadhi ya watu ambao wamepeleka maombi katika mahakama zetu wakitaka kuruhusiwa wajitenge kutoka nchi ya Kenya. Kule pwani tulikuwa na msemo wa “Pwani si Kenya” lakini kwa kuwa tuliheshimu mahakama, wengine wetu tuliamua tuingie katika mchakato wa uchaguzi kwa sababu tulidhani kungekuwa na haki katika nchi ya Kenya. Kwa hivyo, matumizi ya---"
}