GET /api/v0.1/hansard/entries/759281/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 759281,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/759281/?format=api",
"text_counter": 227,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Na hivi tunavyoona ni kwamba, ikiwa mpira uko karibu kuingia kwenye goli halafu unaondoa goli na kuiweka upande mwingine, basi nia yako ni kwamba ule mpira ukipigwa usiingie ndani ya goli. Sababu yao kufanya hivyo ni kubatilisha uamuzi wa Mahakama ya Upeo. Jambo la pili na historia inaweza kutubaini wazi tukiwa hapa ndani ya Bunge hili. Kipengele 2(a) cha Katiba kuhusu Sheria za Uchaguzi, tulisema kuwe na mfumo wa vyama vingi. Utaona ya kwamba, kwa wale watu ambao waliweza kushiriki sana kuleta vyama vingi hapa kulikuwepo mmoja wetu na ndugu yangu Sen. Ndwiga. Juzi tulikuwa tunajadiliana naye akaniambia kuwa alikuwa anatoroka hapa na pale kukwepa polisi wasimkameta kule nyumbani. Leo ninashangaa nikimuona hapa akichangia na kusema sheria hizi zibatilishwe. Aliniambia ya kwamba alikuwa anatafutwa kama panya. Pahali popote alikoenda alitafutwa hadi akalazimika kujitetea. Ndugu yangu alinieleza hayo. Mimi nataka"
}