GET /api/v0.1/hansard/entries/759714/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 759714,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/759714/?format=api",
    "text_counter": 290,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika, ningependa kuunga mkono Hoja iliyoletwa na Seneta Mwaura. Wakenya walitoa maoni yao tarehe nane mwezi wa nane na wakamchagua Rais Uhuru Muigai Kenyatta kwa wingi wa kura million moja nukta nne. Korti imeamua turudie uchaguzi na katika hali ya kurudia, Rais wetu Uhuru Muigai Kenyatta amekubali kurudi apigiwe kura tena na sisi tunahakika na wala hatuna shaka Uhuru Muigai Kenyata atashinda tarehe ishirini na sita na tumejitayarisha kurudi kwa uchaguzi. Bw. Spika, unavyoona nyumba hii wapinzani wengi wako nje barabarani pamoja na wananchi wa Kenya na wameweza kuwapotosha. Mimi ningependa sana wananchi wa Kenya wasipotoshwe na hakuna njia nyingine ambayo tunaweza kuamua uongozi wa nchi ila kupitia kwa kura. Bunge hii imepata fursa ya kurudi mashinani kufanya kampeini na kuwa tayari kufanya kampeini kwa amani. Lakini vile tunavyoona katika mji mkuu wa Nairobi, wananchi wamepotoshwa wakikimbia upande huu na ule. Mwananchi wa Kenya amepotoshwa. Hiyo sio njia ya kuamua uongozi wa nchi ya Kenya. Njia pekee ni ya kuenda kwa kura na kuchagua. Sisi hatuna shaka tukirudi kwa kura Jubilee itashinda na hatuogopi. Wale wanaogopa wamekataa mambo yote. Bw. Spika, Mimi nimeshangaa sana kwamba wanadai hawamtaki Chiloba katika Tume ya Uchaguzi, basi wanamtaka nani? Mambo yote hawataki; hata uchaguzi hawataki. Inafaa waseme kama wanataka “ mkate nusu”. Mkate nusu haupatikani kwa sababu sisi tumeshaenda kwa mashindano na wameshindwa. Ukishindwa, tulia. Mambo ya mkate nusu haiko katika haki hii. Tumesema na tukaamua, mmetuvuta nyuma na tukakubali. Mara hamkutaka Tume ya Uchaguzi ya Kamishna Isaac Hassan ambaye alienda nyumbani na tukaleta Tume nyingine. Mara hii, kila jambo hawalitaki, kama hawataki, nawasihi Wakenya wale waliopotoshwa kwamba nchi ya Kenya ni kubwa kuliko mtu binafsi. Tumefika mahali ambapo wale wanaotaka kutumia demokrasia vibaya wajue kwamba asiyekubali kushindwa si mshindani. Kama hawataki haya mambo yote, basi hawako tayari kushindana na kama hawataki kushindana sisi tayari tuko na Rais."
}