GET /api/v0.1/hansard/entries/760131/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 760131,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/760131/?format=api",
    "text_counter": 222,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, nasimama kuunga mkono Mswada huu. Wakati huu ndiyo mzuri zaidi wa kufanyia sheria hii mabadiliko. Hii ni kwa sababu inajulikana wazi kwamba sheria inatengenezwa wakati mwingi kukiwa na vurugu na vita. Ni vizuri tutengeneze sheria hii wakati huu. Kuna ndugu zetu ambao wanatembea wakisema ya kwamba hakutakuwa na uchaguzi bila mabadiliko ya sheria. Mabadiliko ya sheria hayawezi kufanywa katika maandamano kule Uhuru Park au sehemu zingine zozote isipokuwa hapa katika Bunge ambako tunatunga sheria. Tumekuwa tukiwasikiliza hawa ndugu zetu wa upinzani wakisema maneno mengi. Ijulikane wazi kwamba uvumilivu wetu si uwoga. Sisi ni watu ambao tunapenda sheria na tutaifuata. Hasa Mswada huu unaweka wazi maana ya neno ‘mwenyekiti.’ Hakuna kitu kisichokuwa na mbadala. Ni vizuri kuwa na naibu Mwenyekiti anayeweza kutangaza mshindi wa uchaguzi wakati Mwenyekiti hayuko. Ni vizuri ijulikane ya kwamba mshindi alikuwa ni Mhe. Uhuru Kenyatta. Wanaogopa kwa sababu hata uchaguzi ukifanywa leo, mshindi atakuwa ni Mhe. Uhuru Kenyatta. Itakuwa hivyo hata tarehe 26 Oktoba. Naunga mkono Mswada huu na mambo yote ambayo yametajwa, hasa idadi ya Makamishina inayohitajika kufanya uamuzi. Ni lazima wawe nusu yao ama zaidi. Haya yote ni mabadiliko yanayohitajika. Tusipoyafanya ukienda kortini mahakimu watatoa uamuzi wao na kusema kuhusu mabadiliko ya sheria ambayo sisi Wabunge tunafaa kufanya. Tukitengeneza sheria nzuri ambazo ni wazi, hakuna kitu kitamfanya hakimu---"
}