GET /api/v0.1/hansard/entries/761431/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 761431,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/761431/?format=api",
"text_counter": 1232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "Shukran Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuunga mkono makadirio ya bajeti ya matumizi ya fedha ya mwaka 2017/2018. Imesemwa hapa kwamba ni muhimu kuzingatia matukio katika nchi. Ni wajibu wetu kuangalia upya jinsi tutakavyokabiliana na baadhi ya mambo ambayo yametukumba kama nchi. Nikizungumzia juu ya makadirio ya bajeti hii, ni wazi kwamba wakati huu ni mgumu kwetu Wakenya. Tunashuhudia ugumu wa uchumi wetu ambao sasa hivi haufanyi vizuri. Bunge hili limepewa jukumu kuunda bajeti. Katika hali hiyo, ni muhimu kuzingatia matarajio ambayo wananchi wameonyesha. Upande wa elimu, Ksh23 milioni imetengwa kushughulikia elimu ya bure katika shule za sekondari. Fedha hizi zitashughulikia watoto wa Kenya nzima iwe ni kule Bondo, Siaya, Kisumu, kule nitokako ama kwingineko humu nchini. Kwa hivyo, ijapokuwa wenzetu wa mrengo wa NASA hawamo Bungeni leo, inastahili watupongeze kwa vile tunawafanyia shughuli muhimu ambayo wangekuwa wanafanya wao. Bibilia inasema, mtu asipofanya kazi hastahili The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}