GET /api/v0.1/hansard/entries/761433/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 761433,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/761433/?format=api",
"text_counter": 1234,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "Fedha zingine ambazo imebidi kamati itenge ni zile za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka. Tunafahamu kwamba sasa hivi, tunatarajia kurudi kwa uchaguzi mpya tarehe 26 mwezi huu. Tulipoketi kama kamati kushughulikia masuala haya, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ilikuja mbele yetu na kutupa mahitaji yao. Ningetaka pia ifahamike na Wakenya kwamba kama uchaguzi utafanyika tarehe 26 mwezi huu, ama Novemba, ama Januari ama Februari, uchaguzi ni lazima ufanyike. Inastahili pia ifahamike na Wakenya kwamba kujiuzulu kwa kinara wa NASA katika kinyang’anyiro hakumaanishi alijiuzulu kama mpiga kura. Yeye bado ni mpiga kura. Shughuli hii imechukua shilingi bilioni kumi. Pia, hii inawapatia Wakenya nafasi nzuri ya kuangalia iwapo korti zetu hazingetuingiza katika shughuli za kurudia kura hii. Iwapo huyu babu ambaye analalamika kuanzia asubuhi mpaka jioni hakulalamikia kushindwa, ambapo sasa hivi pia amekataa kurudi kwa uchaguzi; pesa hizi zingetumiwa kwa kazi nyingine kama vile kuendeleza miradi ya barabara, elimu na shughuli nyinginezo muhimu sana katika nchi hii. Pia katika kamati hii tukaonelea kuna pesa wanapewa wakongwe. Na nikisema wakongwe, ifahamike kwamba ni wale maajuza na babu wa miaka 72 kuenda juu. Katika Bibilia inafahamika kwamba mtu ambaye anaishi baada ya miaka 72 anaishi kwa wakati wa kuomba. Kwa hivyo fedha hizi zinashughulikia pia wale watu wamefikisha miaka kama yule babu ambaye ni kinara wa Upinzani."
}