GET /api/v0.1/hansard/entries/761435/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 761435,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/761435/?format=api",
    "text_counter": 1236,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, labda wakati wanasajili hawa maajuza, pia ndugu wetu anaweza kuwa ni baadhi ya wale ambao watafaidika na hizi fedha. Tukiangalia masuala ya usalama, ni Ksh6.9 bilioni imepewa kwa wizara hii. Tunavyoangalia hali ilivyo sasa hivi, tunavyoangalia jinsi utangamano wa Wakenya ulivyo kwa sababu ya hii marudio ya uchaguzi, inahitajika kwamba Katiba ya Kenya inaruhusu kuhakikisha kila Mkenya kwamba serikali itashughulikia usalama wao na usalama wa mali yao. Na hii haiwezi kufanyika iwapo idara ya kusimamia usalama haitapewa fedha jinsi wanavyohitaji. La muhimu zaidi pia, tukizingatia hali ya anga ilivyo nchini sasa hivi tunagundua kwamba baadhi ya maeneo ama majimbo ya nchi hii yamekumbwa na janga baya sana la njaa. Na baadhi ya maeneo hayo ni kama vile pahali ninakotoka. Inahitajika hatua za dharura ili kutatua ama kushughulikia wananchi ambao wanaangamia kwa sababu ya janga la njaa. Haswa, maeneo ambayo yamekumbwa zaidi ni pahali ambapo wafugaji wanatoka. Wafugaji wengi ambao wameketi hapa, wanaotoka Wajir, Mandera, Marsabit, Moyale na kule kwingine kama Narok, Kajiado na mahala pengi, hata mifugo yao sasa imeangamia. Ukitazama chini ya idara ya kilimo, utagundua kwamba Ksh950 milioni, ambayo kwa malengo yangu ni kidogo, itashughulikia kununua wale mifugo kabla ya wao kuangamia ili ipee afueni wale wafugaji ambao kwa sasa hivi hawana la kufanya na hawa mifugo ambao lishe imewaishia, maji hamna, na wamekuwa hohehahe, wasiwe na mbele wala nyuma. Ninapotia tamati, baadhi ya fedha hizi zimewekwa ili kushughulikia usambazaji wa umeme na kununua gesi ya kupika. Tunapozungumza, uhifadhi wa misitu ni muhimu katika nchi hii yetu ili tupate maji na kwa mifugo yetu. Tusiposhughulikia uhifadhi wa misitu, labda itakuwa vigumu kidogo kwa nchi. Kwa hivyo ningeomba Bunge hili, Waheshimiwa walioko hapa na hata wale ambao wataingia kwa muda usio mrefu, waunge mkono makadirio ya matumizi ya Bajeti wa mwaka 2017/2018 ili tuendeleze nchi yetu mbele na kuhakikishia wananchi kwamba kazi muhimu ambayo walitupatia ya kuwawakilisha kwa kweli tumeifanya. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}