GET /api/v0.1/hansard/entries/763199/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 763199,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763199/?format=api",
    "text_counter": 125,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ruweida Mohamed Obo",
    "speaker_title": "The Woman Representative for Lamu County",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "Pia katika huo mradi kwa sasa, watu walisikia kuna malipo. Pengine mtu amekuwa pale kwa miaka mingi na ana ardhi eka kumi. Saa hii katika fidia anaona kuwa ana eka moja. Viongozi waliweka watu wao ili walipwe. Hao wakulima pia waangaliwe. Kuna watu tumeenda kuwashuhudia ambao wanalia. Walikuwa na eka kumi na sasa wako na eka moja. Katika hiyo fidia, watalipwa hivyo kwa sababu wao ni wanyonge na maskini. Wengine ndio wamejipatia hayo majina kuwekwa hapo. Pia kuna wakulima wa Hindi Ward ambao wamekuwa na vita. Kuna wafugaji wanapeleka mifugo kwa mashamba yao na wao wanataka watoke. Wale wafugaji wengine ni wa Lamu na wengine ni majirani wetu. Sasa imekuwa ni vita mpaka shughuli nyingi ni kushughulikia hivo vita. Vita hivyo vinaletwa kwa sababu ardhi kubwa Lamu imekuwa"
}