GET /api/v0.1/hansard/entries/763203/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 763203,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763203/?format=api",
"text_counter": 129,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ruweida Mohamed Obo",
"speaker_title": "The Woman Representative for Lamu County",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Pia kuna wakulima wa watermelon Mpeketoni. Saa zingine zinakuwa nyingi. Naomba pia wakulima hao waangaliwe kwa sababu huwa kilimo ni hasara. Saa zingine hawapati hata kulipa ile deni yao kwa sababu zinakuwa nyingi mpaka hazina soko. Lamu kuna matatizo sana. Katika mambo ya ukulima siwezi kosa kutaja mambo ya ardhi. Tatizo kubwa Lamu ni ardhi. Wakulima wanalima na pengine hawana hati za kumiliki ardhi. Najua tumepitisha hii mikakati ya maswala ya ardhi . Serikali ingilie wapimiwe mashamba ndio wale land grabbers ambao wanachukua ranches wasipate hiyo nafasi maana kuna watu wameishi Lamu kwa miaka mingi kwa vile ni wanyonge. Mara utasikia wanyakuzi wa mashamba wameenda kutwa hati za umiliki ardhi za mashamba makubwa makubwa. Tatizo hili liliibuka wakati wa Serikali ya nusu mkate. Wakati Wizara ya Ardhi ilikuwa kwa nusu mkate, watu walitwa ranches na kwa hivyo kumekuwa na shida kubwa. Hii leo inasemekana eti kuna watu walichukuwa mashamba lakini ukweli ni kwamba visa hivyo ni doti pekee yake. Zile ranches zilizotwaliwa ni nyingi mno. Zilikuwa ekari 350,000. Rais aliziregesha na sasa hivi zimechukuliwa tena. Natumaini sera hii ya ardhi itakagua mashamba ili wale wakaazi wanyonge wa Lamu, wafugaji na wakulima nao wamiliki ardhi."
}