GET /api/v0.1/hansard/entries/763266/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 763266,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763266/?format=api",
    "text_counter": 192,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ali Athman Sharif",
    "speaker_title": "The Member for Lamu East",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza kabisa, nataka nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye aliniwezesha kurudi katika Bunge hili la Kumi na Mbili. Vile vile, nawashukuru wananchi wa Eneo Bunge la Lamu Mashariki kwa kuwa na imani na mimi tena na kuniregesha kuwahudumia kwa miaka mitano ijayo. Bunge hili lajadili Hoja muhimu sana, ni Hoja nyeti na inahusiana na uchumi wetu wa Kenya. Kama tunavyofahamu, ukulima ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu wa Kenya. Lakini, ni masikitiko makubwa kuona, la kwanza, Wabunge wengi hawako kujadili suala hili ambalo ni muhimu katika nchi yetu ya Kenya."
}