GET /api/v0.1/hansard/entries/763268/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 763268,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763268/?format=api",
    "text_counter": 194,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ali Athman Sharif",
    "speaker_title": "The Member for Lamu East",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Katika nchi yetu ya Kenya, sehemu zote ziko na ardhi ya kutosha ya kufanya ukulima. Ni jambo la kushangaza kuona nchi yetu ya Kenya leo inaagiza bidhaa kama sukari kutoka nchi za nje, na ilhali tuko na viwanda na wakulima ambao wako tayari kuifanya biashara hii. Leo ni bidhaa moja ambayo imeletwa hapa na Mhe. mwenzetu. Tatizo moja ni kwamba wakulima hawalipwi pesa yao kwa wakati unaofaa. Na kutokana na haya, inasababisha wakulima hawa kupata hasara, kufa moyo ama pengine inasababisha hali hii ya bidhaa hizi kutoweko katika nchi yetu kwa sababu ya udhaifu kama huu. Sasa tujiulize tatizo hili liko wapi. Tunahitaji kulirudisha wapi tukiwa kama Wabunge ambao wanawakilisha wananchi katika Bunge hili."
}