GET /api/v0.1/hansard/entries/763272/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 763272,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763272/?format=api",
    "text_counter": 198,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ali Athman Sharif",
    "speaker_title": "The Member for Lamu East",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Mimi ningependa kuwaambia ndugu zangu Waheshimiwa kwamba mambo kama haya ni muhimu tuyajadili kwa namna inayotakikana. Tunafaa tujadili ni vipi mkulima atalipwa pesa wakati ameleta bidhaa yake. Ni vipi tutaweza kulizungumzia suala la miwa peke yake kwa sababu uchumi wetu ni ukulima na matatizo yako kila mahali. Leo, Bunge hili litapitisha suala hili la wakulima wa miwa wasaidike kwa namna hii, lakini je, kesho tutarudia tena tuanze kuzungumza na wengine? Naomba ile kamati ambayo itaundwa iweze kuzingatia zile nyanja husika na kuweza kulisuluhisha suala hili la kuhakikisha kwamba nchi hii haiko tena katika ile taswira ya kuonekana kwamba watu wako na njaa, watu wafa na wako na tatizo la chakula. Wakenya wako tayari kufanya kazi hizi za ukulima. Wanachosubiri ni ule usaidizi wa Serikali katika masuala haya. Wale wahusika katika nyanja hizi wahakikishe ya kwamba watu wamesaidika inavyotakikana, na watu wamejiondosha katika ile hali ya kufanya ulafi na ulaghai katika majukumu ya kuendesha masuala kama haya."
}