GET /api/v0.1/hansard/entries/763273/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 763273,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763273/?format=api",
    "text_counter": 199,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ali Athman Sharif",
    "speaker_title": "The Member for Lamu East",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Ni muhimu sana Serikali izingatie wakulima na ihakikishe kwamba imeweza kusaidia viwanda vyote na wakulima wote. Nina imani kubwa litakapofanyika hivyo, basi tutasahau masuala ya matatizo ya vyakula na kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi hii. Leo, kilo moja ya sukari ni mia tatu ama mia nne. Kuna watu wameacha kunywa chai kwa sababu hawawezi kununua sukari. Leo tunajadili vipi mkulima atalipwa pesa yake wakati ameleta bidhaa. Tunamjadili vipi yule anainunua hii sukari ili bei ipungue? Njia ya kuweza kumsaidia yule mwenye kununua bidhaa hii ni kuhakikisha ya kwamba wakulima wamesaidika na tumeweka mambo ya ukulima kisawasawa. Bidhaa zile zinapofika katika mahali pa kutengenezwa, tuhakikishe zimefika kwa mwananchi wa kawaida katika bei ambayo anaweza kununua. Haya ndiyo mambo ambayo nataka tuyazingatie tukiwa kama Waheshimiwa katika Bunge hili. Ni muhimu kuwazingatia Wakenya wa kila aina ya nyanja tukiwa hapa. Kwa mfano, Mkenya anayeuza hii miwa, anayeenda kununua sukari na ambaye anakwenda kulima. Kama nilivyosema, hili ni suala nyeti. Linahitaji kukaliwa vyema na kamati husika na kuhakikisha kwamba yale ambayo tutaweza kuyapitisha hapa katika suala hili pamoja na mengine katika masuala ya ukulima, litamfaidi Mkenya popote alipo."
}