GET /api/v0.1/hansard/entries/763306/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 763306,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763306/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Tuwei",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13436,
"legal_name": "Vincent Kipkurui Tuwei",
"slug": "vincent-kipkurui-tuwei"
},
"content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kuchangia wazo hili ambalo linahusiana na ulipaji wa wakulima wa miwa katika viwanda vyetu. Jambo hili linashangaza sana. Ukulima umekuwa ni hasara. Hasara hii si kwa sababu ya mkulima, bali ni kutokana na usimamizi mbaya wa viwanda vya sukari. Viwanda ambavyo vimefungwa kwa sababu moja ama nyingine ni Miwani, Muhoroni, Ramisi, Chemilil na Nzoia. Ni sababu gani viwanda hivi vya kusaga miwa vinafungwa? Je, ni uongozi mbaya ama ni gharama kubwa ya uzalishaji wa miwa? Sababu ni nini? Serikali imekuwa ikisimama na mkulima, Miswada imewekwa Bungeni, sheria zote zimepitishwa, lakini ni kwa nini mkulima hapati haki yake? Mimi kama Mbunge wa Mosop naona wananchi wangu wameanza kuchukua mashamba yao ya kukuza mahindi na wameanza kupanda miwa. Kampuni ambayo kwa sasa inanunua miwa yetu ni kampuni ya Butali. Kwa sasa, tunaona kwamba kuna faida. Lakini swali The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}