GET /api/v0.1/hansard/entries/763307/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 763307,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763307/?format=api",
"text_counter": 233,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Tuwei",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13436,
"legal_name": "Vincent Kipkurui Tuwei",
"slug": "vincent-kipkurui-tuwei"
},
"content": "ni hili: Kama wale ambao walianza mbeleni viwanda vyao vimefungwa, sababu na kisa ni nini? Vile wenzangu wamesema ni kwamba kuna ufisadi mkubwa katika wizara na usimamizi wa viwanda hivi. Jambo lingine ambalo ningependa kuongelea ni hali ya anga inayochangia katika sehemu zetu. Tunajua kwamba ulimwengu mzima hali ya anga na hali ya kutokuwa na mvua inaharibu na inachangia pia katika mazao ya mkulima; kwamba ekari moja haitaweza kutoa mazao yanayowezesha mkulima yule kupata faida. Jambo hili ni la maana. Inatubidi sisi kama Wabunge tuangalie ni nini tunahitaji kufanya. Kama ni unyunyizaji wa maji katika sehemu zile ziko na maji ili tupate mazao, tupitishe sheria kama hizo. Wakulima wa miwa wanatakikana kusaidiwa na Serikali wapate mbolea kupitia subsidy. Kusaidiwa mbolea na Serikali ili kuimarisha matokeo ama mapato yao. Ni jambo la kushangaza kuona kwamba mkulima ako na miwa na hawezi kumpeleka mtoto wake shule, hawezi hata kulipia mahitaji yake kama binadamu kwa sababu kupanda miwa kwake ni kutoka mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa kumi na nane, ambao ni muda mrefu sana kwa mtu yeyote ambaye anafanya biashara ya ukulima. Sisi kama viongozi na watunzi wa sheria lazima tuwajibike na tuone kwamba mtu yeyote ambaye amekuza chochote ambacho ni cha kumsaidia kwa ukulima apate faida yake na malipo yake apate siku kumi na nne baada ya kupeana mazao yake. Nachukua nafasi hii kumuunga mkono Mhe. Melly kwa wazo hili kwamba wakulima wote wa miwa na hata wa mahindi - Nashukuru kwamba katika ile orodha ya pesa tumepitisha siku ya leo, wakulima wa mahindi na wa kufuga mifugo watafaidika kwa kuwa na pesa za kununua mahindi yao. Hili ni jambo muhimu. Lazima tuweke kwamba mkulima yeyote akipeana mazao yake kwa halmashauri ya miwa ama kwa kiwanda chochote, alipwe baada ya siku kumi na nne. Naunga mkono kwa dhati."
}