GET /api/v0.1/hansard/entries/763315/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 763315,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763315/?format=api",
    "text_counter": 241,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chumel",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 318,
        "legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
        "slug": "samuel-moroto"
    },
    "content": "Ahsante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nami nichangie Hoja iliyoko mbele yetu. Nataka kumshukuru aliyewaza na kuileta mbele yetu. Umesikia jinsi wanenaji wengi wamesema kuhusu Hoja hii. Mkulima wa mahindi, ngano, miwa na hata wafugaji kama mimi ndio wanaoumia kwa Jamhuri yetu la Kenya. Huu ndio wakati Serikali lazima iangalie na ijue kwamba hao pia ni binadamu ambao wana mahitaji yao ya kila siku kama karo ya shule na chakula - maana hao pia ni Wakenya. Wakati mwingi huwa napenda kusema kuwa sisi ni Wakenya, lakini hatuko pamoja ama hatuko na ule usawa. Kuna wale wanaoangaliwa kwa ukaribu sana ilhali kuna wale ambao hata wakifanya maandamano ama walie, hakuna anayewajali wala kuwaangalia. Ningependa kumshukuru yule aliyeweza kuwaza wazo kama hili. Tusiwe tu watu wa kunena hapa na kuachia hapo. Tuwe watu wa kusema na kutenda kwa kufuatilia. Ningependa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}