GET /api/v0.1/hansard/entries/763316/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 763316,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763316/?format=api",
"text_counter": 242,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chumel",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 318,
"legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
"slug": "samuel-moroto"
},
"content": "kuwahimiza wanachama wa Kamati ya Ukulima na Ufugaji tutakapowachagua, wawe macho ili waangalie na kufuatilia kilio cha wakulima. Lazima wazingatie iwapo wanapata haki yao ama la. Nilikuwa katika Bunge la Kumi na Moja na kuna Hoja iliyoletwa kuhusu kilio cha wananchi kuhusu kampuni ya sukari ya Mumias. Sasa, lazima tuangalie maslahi yao. Pia tunafaa kushukuru na kujivunia sana Serikali ya sasa. Wale viongozi wa juu haswa ni watu wenye moyo wa kutaka kusaidia yule mtu wa chini. Lakini, wale wamepewa jukumu la kusimamia ndio wako na malengo tofauti. Tunataka kufanya kazi mpaka yule mwananchi anayelalamika aweze kufurahia uongozi wa nchi yake. Huu ndio wakati tunapaswa kuangalia ili tuone shida iko wapi. Tulikuwa tunauza vitu nje ilhali sasa sisi ndio tunaagiza bidhaa katika nchi yetu. Hili ni jukumu la hili Bunge kuwasaidia wale viongozi walio na nia. Nilihudumu enzi za Moi na Kibaki lakini Rais wa sasa na Naibu wake wanakaribia wananchi. Nikisema hivyo, najua wengine hawaelewi ni kwa nini. Wale wameteuliwa jana wanafikiria ile vita tunakuwa nayo hapa na mrengo wa Upinzani. Mrengo wa Upinzani haupo kwa sasa bali nafikiri ni mchezo tu. Kuna wakati Upinzani ulikuwa Upinzani. Kwa sasa, kuna wale wanateremka kukutana na watu wao kila siku. Hii wiki wamekuwa Mombasa.Wananchi pale wanalilia vitu vyao vidogo. Jana, Rais mwenyewe aliweza kutoa vyeti kwa ajili ya vitu vidogo vidogo kama misitu katika ile hali ya watu kung’ang’ana hapa na pale. Nafikiri Kamati za Bunge kwa sasa ziko na nguvu kushinda pale awali. Wale mawaziri walioteuliwa walikuwa na nguvu sana. Lakini sisi hapa hatujaanza kuchukua ile sehemu yetu ya kufanya kazi na kuona kitu gani haswa kitafanyika. Naibu Spika wa Muda, yule tumemwekea jukumu kama Waziri wa Kilimo, Ufugaji na Maendeleo anatoka eneo tunalolizungumzia.Yeye binafsi anaweza kuona vile miwa inaharibiwa. Anaweza akatafuta muda ili apitie pale na kupata fursa ya kuzungumza na wakulima wanaoumia. Hatoki mbali na sehemu tunayoiongea kuhusu. Amewahi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Kenya Seed. Kwa hivyo, lazima asikize tunachosema hapa. Hatuwezi tukampa mtu kazi tukiwa na nia nzuri tukitarajia kwamba atatusaidia halafu hatusaidii. Ni sisi ndio tunapitisha hata mawaziri hapa. Hata wale wa upande wa Upinzani, majina yao yanapitia hapa. Kwa hivyo, ni lazima wajue kwamba sisi ndio tunabeba mzigo wa wananchi. Tukisema tunataka hivi ni lazima watusikize. Hivi sasa, ukitaka kuwaona, huwezi kuwaona. Wanakuwa wakubwa kuliko yule Rais ambaye wakati mwingine tunashikana mkono na kucheza naye. Kwa hivyo, nashukuru sana Lake Victoria North Water Services Board. Wamejaribu sana kiasi ya kwamba wanatufikia mahali hawatakiwi kuja kwetu. Mhe. Lagat ndiye Mwenyekiti na anaelewa vile watu wanaumia. Lakini kuna ile ya Rift Valley Water Services Board na hatumuoni Mweneykiti ilhali sisi ndio watu wa Bonde la Ufa. Nadhani wanataka tuwe tukizunguka katika maofisi yao ndio watoke na wasaidie wakulima. Hakuna kitu ambacho kinafanyika bila maji. Kule ninakotoka kuna jina tumekuwa tukiwekewa kama cattle rustlers. Ni shida wakati mtoto analia usiku wote. Keshoye ni lazima upambane uende kwa jirani uombe ng’ombe moja huku ukitafuta mboga ya watoto. Lakini sasa Serikali hii imeleta faida na huduma karibu na watu. Wanatakiwa kuleta maji halafu unapata wanapotea. Sisi hatuwezi kulaumu huko juu. Tunaanza kutafuta hapa chini tukiuliza: “Hawa ni akina nani?” Kwa hivyo, ninashukuru sana. Tuna jukumu. Najua kuna wenzetu wengine wanaofikiri kwamba wako katika jeshi. Hiyo fikra itoke hapa ndiyo tuweke fikra zetu pamoja. Mungu awabariki."
}