GET /api/v0.1/hansard/entries/763749/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 763749,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763749/?format=api",
    "text_counter": 42,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Ahsante Bw. Spika. Ningependa kuchukua fursa hii kupeleka risala zangu za rambirambi kutoka kwangu, familia yangu na watu wa Tana River kwa jumla kwa kifo cha Gavana wa Nyeri. Ningependa kuwapa pole Serikali na watu wa Nyeri. Ningependa pia kumpa pole Seneta wa Nyeri, ambaye tuko naye hapa. Tutasimama na nyinyi wakati huu mgumu amba oGavana wetu ametuacha. Naomba kwamba wakati huu usiwe wa siasa, bali uwe wakati wa kuomboleza na kutuleta sisi sote pamoja. Huu ni wakati wa kupeana moyo kwa watoto wake, familia yake na hasa kwa mtoto wake ambaye ana fanya mtihani wa kitaifa. Tunampa moyo na pole wakati huu mgumu."
}