GET /api/v0.1/hansard/entries/763764/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 763764,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/763764/?format=api",
    "text_counter": 57,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "November 7, 2017 SENATE DEBATES 11 Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Alihusika pakuu. Kwa hivyo ni mtu ambaye amechangia katika nchi hii yetu ya Kenya. Pia nasema pole kwa watu wa Nyeri na hasa familia yake na mtoto wake ambaye anafanya mtihani wake wa kidato cha nne. Haya mambo yanapotokea yanatusumbua sana hasa wakati ambao nyoyo za watu wa Nyeri hazijatulia kwa sababu tayari walikuwa wamempoteza Gavana wao wa hapo awali, Bw. Gachagua. Tena Gavana mwingine ameaga. Kwa hivyo tunapaswa kujiweka katika Bwana. Tumtegemee Mwenyezi Mungu. Nina imani na hakika ya kwamba tukimwomba Mwenyezi Mungu mambo haya yataendelea kuwa sawasawa na hatutakuwa na hii shida tena. Lakini kwa watu wanaohusika, mambo ya barabara yaangaliwe kwa sababu ajali zimekuwa zikitokea sana katika barabara zetu. Wakati mwingine shida hutokea kwa sababu ya mashimo yaliyo barabarani. Dereva anagonga shimo halafu gari linakosa mwelekeo. Kwa hivyo hili jambo linapaswa kuangaliwa. Mwisho nawaambia watu wa Nyeri na Kenya nzima pole kwa sababu ya kupatwa na hilo pigo la kumpoteza Gavana wetu. Marehemu Gavana Gakuru alale mahali pema peponi."
}