GET /api/v0.1/hansard/entries/7638/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 7638,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/7638/?format=api",
"text_counter": 301,
"type": "speech",
"speaker_name": "Bw. Bett",
"speaker_title": "The Minister for Roads",
"speaker": {
"id": 157,
"legal_name": "Franklin Kipng'etich Bett",
"slug": "franklin-bett"
},
"content": " Bw. Naibu Naibu Spika wa Muda, ni ukweli Rais alizindua ujenzi wa barabara katika eneo hilo. Hata hivyo, Bw. Kutuny ana haki ya kuuliza Swali lake hapa Bungeni. Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba kujibu. (a) Wizara yangu haijaweka lami barabara mpya katika eneo la Cherang’any mwaka huu. Hata hivyo, kupitia Kenya Rural Roads Authority (KeRRA), tumetoa kandarasi ya kujenga upya barabara ya Eldoret-Ziwa-Kachibora (D328) na Kachibora- Moi’s Bridge (D330/E334). Vile vile, kupitia Kenya National Highways Authority (KeNHA), Serikali imetenga Kshs160 million kugharamia ukarabati wa barabara ya Kitale-Sibanga (C48). (b) Kupitia Kamati ya Barabara ya Eneo Bunge la Cherang’any (CRC), Kshs2,272,400 zimetengwa kukarabati kilomita 20 za barabara za Maili Saba-Sibanga (D330) na Kaplamai-Kachibora (E328) mwaka huu wa matumizi ya pesa 2011/2012. Kazi hii itaanza baada ya mvua kupungua. Pia, kupitia KENHA, Kshs18 million zimetengwa mwaka huu wa 2011/2012 ili kugharamia ukarabati wa sehemu kadhaa za barabara kati ya Kachibora na Kapcherop. Shughuli ya kutoa kandarasi imeanza na tunatarajia kwamba kazi yenyewe itaanza mwezi wa Disemba mwaka huu. (c) Ni kweli kwamba mvua inayoendelea kunyesha katika eneo la Cherang’any imeharibu sehemu za barabara kadhaa ikiwa pamoja na zile zilizokarabatiwa wakati wa matumizi ya pesa 2010/2011. Mwaka huu (2011/2012), Serikali kupitia kamati ya Eneo Bunge la Cherang’any (CRC), imepanga kutumia Kshs30 milioni kukarabati kilomita 299 za barabara katika eneo hilo. Kazi ya kukarabati barabara itaanza baada ya kumalizika kwa msimu huu wa mvua."
}