GET /api/v0.1/hansard/entries/7639/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 7639,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/7639/?format=api",
    "text_counter": 302,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda nimemvulia kofia Waziri kwa kujibu Swali hili katika lugha sanifu ya Kiswahili. Kwanza nataka kushukuru pia Serikali kwa kuzindua ujenzi wa barabara kadha wa kadha katika sehemu za North Rift. Barabara ambayo kandarasi tayari imetolewa inaanzia Chepkoilel-Ziwa-Kachibora. Barabara hii inaenda mpaka Kitale. Pia, amesema kwamba kandarasi ya ujenzi wa barabara kutoka Sibanga hadi Kitale tayari imetolewa. Hata hivyo, hakuna karandarasi iliyotolewa ya ujenzi wa barabara ya Kachibora mpaka Sibanga. Ningependa Waziri aeleze Bunge Serikali ina mipango gani ya kukarabati barabara hii ili iweze kutumika."
}