GET /api/v0.1/hansard/entries/764878/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 764878,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/764878/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Obo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Kama utaniruhusu, ningependa kutoa rambirambi zangu kwa jamaa na marafiki wa Gavana wa Nyeri. Mimi na watu wa Kaunti ya Lamu tunasema pole. Pia Lamu tumekuwa na mkasa mdogo na ningependa kutoa rambirambi zangu. Kuna mgonjwa wa akili aliyekuwa anatembea msituni. Maafisa wa KDF walimpiga risasi kisha wakaandika wameua gaidi wa Al-Shaabab . Tunatoa pole na tunaomba wahusika waombe msamaha kwa sababu familia ina uchungu sana na sisi kama viongozi wa Lamu tunajaribu kuweka jamii na maafisa wa usalama wawe karibu na wasiwe mbali sana ili wakiona mtu anapita ambaye hawamjui wapeleke habari. Hata hivyo mambo haya yakiendelea kwamba watu ambao hawana hatia wanauawa hiyo chuki inaendelea na hata wakiona wahalifu hawawezi kusema. Haya mambo ya pension in mazuri na itasaidia maana hata tunaogopa. Kila anayesimama anatupatia mfano wa kusema wale waliokuwa hapa na sisi ni wageni tumeingia. Tunaogopa na tumeingiwa na uoga tusije tukatoka hivi hivi na ukiona mambo yanavyoendelea hali saa hii ni ngumu na mishahara imekatwa. Tunafikiria kwenda kuvaa badge turudi kwa kurusha ndege au kufanya kazi zingine. Hata hivyo naona muda hautoshi. Tunafaa tuhudumie jamii. Kwa hivyo mimi ninaunga mkono sana mambo haya ya pension . Sijui pension kwa Kiswahili. Asante."
}