GET /api/v0.1/hansard/entries/764946/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 764946,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/764946/?format=api",
"text_counter": 164,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwale",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13311,
"legal_name": "Nicholas Scott Tindi Mwale",
"slug": "nicholas-scott-tindi-mwale"
},
"content": "Ahsante Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ili nichangie Hoja hii ya kupitisha majina ya wanakamati ambao watatusaidia kama Wabunge katika malipo baada ya kustaafu. Kwanza kabisa, ningependa kusema kuwa hili jambo limechelewa kidogo kwa sababu kuna wenzetu ambao walipoteza viti vyao na wanateseka kule nje. Kwa hivyo, sina pingamizi lolote. Naunga mkono ili majina haya yapitishwe. Siwajui waheshimiwa hao kwa kukutana nao, lakini naamini kwamba, wale wamechagua majina hayo wanawajua na wanajua kwamba watatekeleza majukumu yao kwa njia ambayo itafaidi waheshimiwa. Katika hili Bunge, wale ambao tumekuja kwa mara ya kwanza tumefika karibu asilimia 60. Tunaambiwa kwamba kurudi hapa ni vigumu sana. Tungeomba sana haya mambo ya malipo baada ya kustaafu ianze baada ya muhula wa kwanza wala siyo baada muhula wa pili. Ianze baada ya Mbunge amefanya kazi katika muhula wa kwanza. Jambo lingine ni kwamba, hakuna haja ya kuita mtu Mheshimiwa na unamnyima malipo baada ya kustaafu halafu anaanza kuzunguka katika Bunge kuomba hayo malipo. Kama mtu ni mheshimiwa basi apewe heshima yake. Kama hajafaulu katika kura, apewe malipo yake ya baada kustaafu na mshahara wake wa mwisho. Jambo la waheshimiwa kuja na kuanza kuzunguka hapa si zuri. Jambo hili kuhusu malipo baada ya kustaafu halifai tu kuongelewa Bungeni. Hii ni shida ambayo kila Mkenya ako nayo. Nikirudi katika eneo langu la Bunge la Butere, niko na wale watu waliostaafu na wanauliza kwa nini Serikali haijawalipa malipo yao baada ya kustaafu. Nikienda katika hiyo ofisi naambiwa nitoe stakabadhi nyingi. Ningependa kusihi Serikali na hii kamati, malipo baada ya kustaafu yachukuwe muda mfupi kutayarishwa. Mambo ya kuzungushwa huku na huku haifai kabisa katika nchi yetu ya Kenya. Nikimalizia, ningependa kutuma risala za rambirambi kwa familia ya Gavana Wahome Gakuru aliyetuacha. Nilimjua kama rafiki. Tumejuana kidogo. Angebadilisha maisha ya Wanyeri. Kwa hayo machache, ningependa kuunga mkono Hoja hii inayopitisha majina ya waheshimiwa watakaounda kamati ya kushughulikia malipo ya baada ya kustaafu. Ahsanteni."
}