GET /api/v0.1/hansard/entries/764995/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 764995,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/764995/?format=api",
    "text_counter": 213,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Hakuna jambo la muhimu kama kuwa na mipangilio kikamilifu kuhakikisha kuwa nchi yetu na miji yetu imepangwa kisawasawa, na haswa, katika hali ya mambo ya ujenzi wa nyumba za kuishi na za kufanyia shughuli za kibiashara. Naunga mkono Hoja hii ya Ruwaza ya Serikali ya Kenya ya kuhakikisha kuwa mipangilio hiyo inafanywa kisawasawa. Miji ya Nairobi, Mombasa, Kisumu na Eldoret ni miji ambayo imepitwa katika mipangilio yao kwa sababu ya idadi ya watu wale ambao wameongezeka katika miji hiyo. Kwa hivyo, kuna umuhimu kuwa miji mingine pia iweze kupangwa kikamilifu ili iweze kupunguza idadi kubwa ya watu inayokwenda kwenye miji hiyo minne. Katika Kenya hii, hauwezi kusema utafanya mipangilio kama suala la ardhi halitakuwa limetatuliwa. Hata miji mingi ikitaka kuwa na mipangilio mizuri, tatizo kubwa lililoko ni ardhi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}