GET /api/v0.1/hansard/entries/764996/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 764996,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/764996/?format=api",
"text_counter": 214,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "ambayo imepeanwa kiholelaholela. Serikali ya Kenya inatumia pesa nyingi sana kununua ardhi kutoka kwa wale ambao walipatiwa ardhi hiyo kiholela, ili waweze kupanga mipangilio na hata kujenga sehemu ambazo zitatumika na umma - haswa ofisi ambazo zinatumika na Serikali kuu na hata serikali za ugatuzi. Kuna mambo ambayo Serikali hii, kupitia mipangilio yake, inaweza kupanga. Ingeanza na kulitatua kikamilifu suala la ardhi. Mipangilio bila ardhi haiwezi kusonga mbele. Serikali yetu haiwezi kuendelea kulipa pesa zile nyingi inazolipa ili kupata ardhi ya kutosha kuweza kufanya mipangilio hii. Mipangilio hii ni lazima. Ili Hoja hii ipite, ni lazima Tume inayosimamia masuala ya ardhi iweze kufanya kazi kwa ukaribu sana pamoja na Serikali kuu, Wizara ya Ardhi, Wizara ya Mipangilio pamoja na Wizara inayosimamia maendeleo katika maeneo ya mjini. Serikali yetu inavyozidi kufanya kazi hizi na kupanga mipango hii, itaweza kuendelea mbele namna gani kama suala la ardhi halitakuwa limetatuliwa? Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii."
}