GET /api/v0.1/hansard/entries/765128/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 765128,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/765128/?format=api",
"text_counter": 84,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kanini Kega",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1813,
"legal_name": "James Mathenge Kanini Kega",
"slug": "james-mathenge-kanini-kega"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii ili niomboleze na familia ya mwendazake Gavana wetu wa Nyeri. Kwa niaba yangu, familia na wale ninaowaakilisha katika eneo Bunge la Kieni, ninatoa rambirambi zangu kwa familia, jamaa na marafiki wa mwendazake gavana wetu. Alfajiri ya leo, tulipata habari ya kwamba Gavana wetu alihusika katika ajali ya barabara ambayo tulifikiri ni ajali tu ya kawaida. Na muda si muda, tukaambiwa ametuacha. Ni pigo kubwa kwa watu wa Nyeri tukiangazia kwamba marehemu Mhe. Gachagua, ambaye alikuwa gavana wa kwanza, alituacha miezi tisa iliyopita. Kwa hivyo, ni wingu kubwa la simanzi ambalo liko katika Kaunti yetu ya Nyeri. Lakini kwa sababu sisi wote tukiwa kule ni wakristo na wacha Mungu, tunasema kwamba Mungu ndio anajua wakati mtu anazaliwa duniani na atakapoondoka duniani hasa kwa sisi viongozi. Waswahili husema; “Tenda wema nenda zako.” Wakati tuko katika dunia hii, ni vizuri tuwe ama matendo yetu yawe ni matendo mema kwa sababu muhula wetu hapa ni mfupi sana. Kwa hivyo, wale ambao wanamjua wanajua kwamba alikuwa msomi na mpenda watu. Tulikuwa tunafanya kazi pamoja wakati huu wote tukiwa viongozi wa Nyeri. Wakati alipokuwa akitawazwa kama Gavana wa Nyeri, sisi sote, kama viongozi, tuliungana na kusema kwamba tunataka Nyeri iende mbele; lakini hayo yalikuwa ni yetu. Mungu alikuwa na mipango mingine."
}