GET /api/v0.1/hansard/entries/765174/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 765174,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/765174/?format=api",
"text_counter": 130,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chelule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13126,
"legal_name": "Liza Chelule",
"slug": "liza-chelule"
},
"content": "Ahsante sana, Bw. Spika kwa kunipa nafasi nitume risala zangu za rambirambi kwa familia ya marehemu Gavana wa Nyeri. Tunapotafakari, kuna sababu kubwa sana ambayo ilifanya wakaaji wa Nyeri kumchagua Dkt. Gakuru kama kiongozi wao. Kama wakaaji wa Jimbo la Nakuru, tunawaombea sana kwamba wakati huu wa majonzi, Mungu aweze kuwasimamia, kulisimamia Jimbo la Nyeri na kuisimamia familia, hasa kijana wake ambaye anakalia mtihani wake. Mungu aweze kusimama naye na kumpa nguvu ili aweze kustahimili shida ambayo imeipata familia yake. Pia, natoa risala za rambirambi kwa watu waliotoka katika kijiji changu na Jimbo la Nakuru ambao walipoteza maisha yao katika ajali ambayo ilitokea katika barabara ya Salgaa inayojulikana sana kama barabara mbaya ambapo tumepoteza watu wengi sana. Pia, natoa risala zangu za rambirambi kutoka Jimbo la Nakuru kwa wale wote ambao walipoteza maisha yao katika ajali ya ndege ambayo ilitumbukia ndani ya Ziwa la Nakuru. Watu wawili walipatikana lakini watatu hawajapatikana mpaka sasa. Ni maombi yetu kwamba Mungu aweze kuzisimamia familia zao na kuwapa nguvu. Ninawaza kwamba Bunge hii pia iangalie vile tutatatua ama kuchunguza mambo ya ajali ambazo hutokea kila mara. Nafikiri tukifanya uchunguzi kuhusu ajali zinazotokea, itakuwa ni njia moja ya kupunguza ajali katika nchi yetu. Kama Bunge, bado tutarudi hapa tuongee tena na kuona vile ambavyo mambo ya ajali yanaweza kutatuliwa katika nchi yetu. Poleni sana kwa wale wote ambao walipatwa na ajali na familia zao."
}