GET /api/v0.1/hansard/entries/765327/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 765327,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/765327/?format=api",
    "text_counter": 283,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chumel",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 318,
        "legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
        "slug": "samuel-moroto"
    },
    "content": "Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ili nami pia nitoe wazo langu juu ya Hoja ambayo iko mbele yetu. Nalaani kitendo cha kuwaua wanyama. Ningependa kuwauliza wale ambao wanahusika na masuala ya wanyama, kama wale wanaopigania haki za kibinadamu na wengine kuangalia suala hili. Hii si mara ya kwanza kitendo kama hiki kimetendeka katika eneo hili. Wengine wetu tumetoka mahali ambapo kumekuwa na shida ya usalama kwa muda mrefu kama vile Turkana, Pokot, Karamajong, Sebei hata upande wa Trans Nzoia. Hatujafika kiwango ambacho tumeona operesheni kama ya 1984 iliyoitwa Operation Nyundo ambapo walikuwa wanatafuta watu. Hawakukusanya ng’ombe na kuwapiga risasi. Najulisha wenzangu wajue kwamba huu si ule wakati wa zamani. Tuko na Katiba mpya. Ule unyanyasaji wa wafugaji tangu wakati wa ukoloni umeisha. Ni lazima tuwaheshimu wafugaji. Ripoti ya Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano, ambayo imetajwa na mmoja wetu, iliweka wazi shida za eneo hili."
}