GET /api/v0.1/hansard/entries/765329/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 765329,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/765329/?format=api",
"text_counter": 285,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chumel",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 318,
"legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
"slug": "samuel-moroto"
},
"content": "Wengine wetu tumefanya kazi kwa Serikali na tumehusika na masuala ya usalama. Kuna fununu kwamba ng’ombe waliuliwa kwa sababu wakora waliwatumia kama kinga. Mbona hakuna mkora hata mmoja ambaye alipigwa risasi wakati ng’ombe 300 waliuliwa? Hao wakora wako wapi? Hata mtu mjinga anaweza kuuliza: Mbona ng’ombe 300 waliuliwa bila mkora hata mmoja kupatikana? Halafu tunaambiwa wakora walitumia ng’ombe kama ngao. Kenya ni yetu sisi wote. Hakuna kabila lililo bora kuliko lingine. Tuko sawa sote. Naomba tuteue kamati ya Bunge ili ichunguze kitendo hiki na ilete ripoti ili tujue makosa yalikuwa wapi. Kitendo hiki kilifanyika mara ya kwanza na watu wakafikiria kitapita. Baadaye, wanyama wakauliwa tena. Hakuna mtu amesimama hapa kusema mkora asipigwe risasi. Lakini kwa nini wanyama wauliwe? Mbona wanyama wa kundi moja waliuliwa na sio wa kundi lingine? Kwani hao pekee ndio walikuwa na ng’ombe huko? Mbona hatujasikia ng’ombe ameuliwa hata wa Mbunge wa eneo hilo? Mbona ngómbe wa watu wengine ndio wanauliwa? Kama ni ng’ombe wangu wameuliwa, watu wasikie hata ngómbe wa Moroto wamepigwa risasi na wa wengine. Lakini katika laini moja pekee yake ndio watu wanazungushwa. Hiyo ndio italeta hasira. Sisi ni wafugaji. Ninataka niiambie Serikali kwamba watatuzungusha kidogo lakini tutaungana na mapambano yatakuwa kati ya wafugaji maskini na matajiri. Mungu atawasaidia maskini ambao ni sisi, wale ambao tunanyanyaswa mchana na usiku. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}