GET /api/v0.1/hansard/entries/765346/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 765346,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/765346/?format=api",
    "text_counter": 302,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Teiyaa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13239,
        "legal_name": "Janet Marania Teyiaa",
        "slug": "janet-marania-teyiaa"
    },
    "content": "Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nami nichangie kwa mjadala huu. Ninataka kumpongeza Mhe. Peris Tobiko, Mbunge wa Kajiado Magharibi, kwa kuleta Hoja kama hii. Hili ni jambo mbaya sana. Ninaanza kwa kukemea sana kitendo kama hiki. Kuamuka na kukuta ng’ombe wakilala chini na sio kiangazi imefanya wakufe ni uchungu sana. Ni vibaya sana kuua ng’ombe ambao hawawezi kujitetea ilhali hakuna ngo’mbe alijipeleka hapo. Wangetafuta mahali pa kuwapeleka badala ya kuua ngombe. Hakuna siku ambayo ng’ombe atachukua risasi apige binadamu. Kwa hivyo, hicho ni kitendo cha kukemewa. Tunajua kwamba wafugaji hutegemea wanyama kupeleka watoto shule na chakula. Kwa hivyo, tunajua kwamba ng’ombe wakiisha hakutakuwa na maisha na watu watarudi kuwa masikini, ilhali hao ng’ombe wangewasaidia kusomesha watoto wao na waishi vizuri. Tunataka kama ni askari wamefanya hicho kitendo, washikwe. Hili ni jambo ambalo halikubaliki na hatuwezi kusimama tukiona mabaya yakitendeka. Haya ni mambo ambayo yametupata mara nyingi kama wafugaji. Tunaongea kuhusu Laikipai kwa sababu leo imefanyika huko lakini hiki ni kitendo ambacho kimefanyika mara nyingi kwa jamii ya wafugaji. Hivi juzi, kule Kajiado tulilia kwa sababu ya ng’ombe ambao walipigwa mnada nchini Tanzania. Kuongea hapa hakutatusaidia. Ni lazima tutafute suluhu ya kudumu. Ninaunga shinikizo la kuundwa kwa kamati ya kuchunguza mambo haya. Pia, ninaunga mkono pendekezo la kuwalipa fidia wale watu amabo ng’ombe wao waliuliwa na polisi. Kuna watu ambao wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi ilhali hawakuwa na hatia. Familia za watu hao pia zilipwe fidia. Pia, tunafaa kuelewa masuala ya kiangazi. Tunapoambiwa hapa ni pabaya, pia tuelewe kwamba hakuna kiongozi anayewambia wananchi waende wakaharibu shamba za watu wengine. Hakuna kiongozi atakayeamrisha askari wawapige ng’ombe risasi. Kwa hivyo, ni lazima jamii ielewe kwamba wale waliotekeleza mauaji ya ng’ombe hao ni wahalifu. Hakuna vile kiongozi anaweza kuwatuma askari waende wakawaue wanyama ambao ni tegemeo la kila mfugaji. Kwa hivyo, tumekataa jambo hili na tunasema ni lazima watu walipwe fidia. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}