GET /api/v0.1/hansard/entries/765373/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 765373,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/765373/?format=api",
    "text_counter": 329,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Kwa hivyo, tunaona hakuna haja ya kupiga kelele. Ningependa kuwaambia ndugu zangu ambao ni viongozi wa Laikipia kuwa ni lazima tukae chini na tujue haya mambo ya Laikipia yalianza namna gani. Hii si mara ya kwanza taabu imetokea Laikipia. Imetokea mara mingi na tukajaribu kuleta peace caravan na itapoa. Mambo ya kupiga ng’ombe risasi ilianza miaka mitatu iliyopita. Ukame huwa kila wakati na kila wakati tunaenda Laikipia kutafuta nyasi. Hatuendi kuchukua shamba ya wenyewe kwa nguvu, kuvunja ama kubeba vitu. Watu wanaenda kununua nyasi kwa wale ambao wako kwa mashamba. Mambo ya kuleta askari kupiga ng’ombe risasi ilianza miaka mitatu iliyopita. Ng’ombe wengi walipigwa risasi na tuko na ushahidi wa kutosha. Pia, tuko na ushahidi wa watoto na kina mama kupigwa risasi. Mimi sifurahishwi na mambo ambayo viongozi wetu wengine wanasema. Ni kweli askari wameuawa. Hatukatai. Lakini nani ameua askari? Ungeenda kushika mwenye ameua askari na si ng’ombe. Tunajua askari wamekufa lakini yule amewaua angeshikwa. Kwa nini wanapiga ng’ombe risasi?"
}