GET /api/v0.1/hansard/entries/765374/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 765374,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/765374/?format=api",
"text_counter": 330,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Kile hatuwezi kukubali pia ni kile IGP, Mr. Boinett, amesema kuwa watu wanaenda kushika ng’ombe na ndio wanapigwa risasi. Hatujawahi kumpata mtu ambaye ameenda kushika ng’ombe na akafa naye. Kuna shida ya ng’ombe mahali kwingi. Pia, maafisa wa Serikali ambao wako kule wako na shida nyingi. Kama wanasusia Serikali, wasisusie Serikali kwa kutumia Wasamburu. Wasusie Serikali kwa njia nyingine kwa sababu kuna mambo mengi pale. Kwa hivyo, dada zangu viongozi, kuna mambo mengi pale. Tushaajua na tushaakaa mara tatu na lazima turudi tukae chini tujue ni nini kinaendelea. Naomba viongozi wa Laikipia tusitie hili jambo moto sana isionekane kama kwamba Wasamburu wanatolewa Laikipia. Tukifuata mkondo huo, tutaleta taabu Kenya nzima. Hatuulizi kwa sababu gani Wasamburu wako pale. Wasamburu wa Laikipia ni wazaliwa wa huko na wako na ng’ombe. Si kwamba ngómbe wa Wasamburu pekee ndio wamepigwa risasi. Hata ng’ombe wa wale wanaoishi huko wamepigwa risasi na tuko na ushahidi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}