GET /api/v0.1/hansard/entries/765375/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 765375,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/765375/?format=api",
    "text_counter": 331,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Naomba sisi viongozi tujaribu kufuatilia kujua ni nini kilifanyika huko Laikipia. Wale ambao ng’ombe wao waliuliwa wako na shida nyingi sana. Kwa mfano, watoto wao hawawezi kwenda shule. Katiba yetu inawachunga wananchi na mali yao. Lakini sasa mali imeharibiwa na Wasamburu hawana shamba ya kwenda kuchuna majani. Ng’ombe wao ndio majani chai, sukari, mahindi na miraa. Kwa hivyo, ni lazima tujue ya kuwa ng’ombe ndio tegemeo la wafugaji. Ni ngómbe wametulea sisi mpaka tukawa hivi na bado wanatulea. Tutafute njia ya kisheria ya kutatua jambo hili. Naunga mkono kuundwa kwa kamati ya Bunge ya kuchunguza mambo yanayoendelea. Naomba Mbunge wa eneo hilo na Wabunge wote wa Laikipia tukae chini bila kuchelewa kwa sababu tumepata ujumbe kwa simu zetu ukitangaza eti Wasamburu warudi kwao. Hatuwezi kukubali jambo kama hilo."
}