GET /api/v0.1/hansard/entries/766963/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 766963,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/766963/?format=api",
"text_counter": 1568,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Obo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Mhe. Spika wa Muda, nakushukuru sana kwa kunipatia hii nafasi nichangie Hoja hii na kuiunga mkono. Ni vizuri kuwa na mpangilio ili tufaidike kutokana na lile tunalotafuata. Mwanzo, ningependa kuishukuru ile kampuni ya Zarara ambayo iko Lamu. Wamejitahidi sana. Wanakwenda mashinani kuzungumza na jamii. Kwa hivyo, jamii katika Lamu Magharibi, na haswa katika Wadi ya Faza, wanajua kile kinachoendelea. Naomba pia kampuni zote zinazokuja Lamu kwa chochote wahusishe jamii vizuri. Pia, kile kinachopatikana kutokana na kuchimbwa kwa madini kiwe kinafaida jamii maana vitu vingine kama ule mradi wa makaa Lamu umeleta shida sana. Viongozi waliokuweko labda waliwaonyesha manufaa; lakini sisi tulioingia Bungeni, tunaomba pia tupitie mpangilio wao watuonyeshe kama huo mradi una manufaa kwa jamii ama hauna. Tunaomba watupatie muda, kama viongozi, ili tufanye utafiti wetu. Wasitupeleka haraka vile huo mradi unavyoenda. Tunataka viongozi na jamii mashinani wahusishwe vizuri. Ikiwa kitu kinafaida, watueleze vyema. Vile vile, kama kitu hakina faida, tuambiane kinaga ubaga. Asante, Mhe. Spika wa Muda."
}