GET /api/v0.1/hansard/entries/766978/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 766978,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/766978/?format=api",
"text_counter": 1583,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13275,
"legal_name": "Rehema Hassan",
"slug": "rehema-hassan"
},
"content": "hivyo mifugo wetu kule kwa bahati mbaya wakiteleza wanakufa kwa sababu ya maji ambayo yako ndani ya hayo mashimo. Hata wanadamu hufa kwa njia hiyo. Pili naomba tujumuishe katika hii sera sheria kwamba hao matajiri ambao wanachimba yale mawe waweze kuwafanyia wenyeji maendeleo. Hiyo itakuwa kama shukrani ili waweze kufaidika kutokana na ile rasilimali. Hakuna chochote wanatufanyia, ila wao ni kuchimba mawe, kuuza simiti na kuendelea kufungua mitambo huku na kule. Sisi tunazidi kuwa maskini tu. Tukijaribu kuzungumza nao hawaonyeshi huruma na angalau waseme hawa tumewaharibia ardhi yao wacha hata tujenge hospitali ama zahanati ya kuwasaidia wenyeji ndio washukuru. Hawafanyi hivyo. Kwa hivyo, naomba tuongeze katika sera hii kwamba wakichimba madini sharti wafaidi wenyeji pia. Iwe kama lazima kuwa wakishachimba yale mawe wajenge hospitali, shule ama matenti. Waaache kuwa wajeuri. Tumejaribu kuwafuata wazibe machimbo yao lakini wao hutuambia eti hatuwezi kuwapeleka popote. Pia, naomba watu wa National Environment Managment Authority (NEMA) watembee waangalie kule uchimbaji unakofanyika. Je, hiyo ardhi ama hiyo sehemu inalindwa kivipi kwa sababu kuna mashimo kila mahali? Kule kwetu Chardende wameweka mashimo. Nanighi pia wameweka mashimo wakaacha. Saa hizi wamesonga na kufika karibu Madogo. Wanachimba mashimo wakiyaawacha. Hiyo ni ardhi yetu wanatuharibia. Si kuwa sisi ni maskini hatuwezi kuja kuanzisha miji huko. Wanatuharibia ardhi. Twaweza kuja tukaanza miji. Tunataka kukua kama kaunti pia. Kwa hivyo, watu wa NEMA pia wawangalie hao watu wa kuchimba gypsum kule Chardende na Nanighi. Wameenda mpaka sehemu inaitwa Amare. Wanachimba mashimo tu wakiyaacha kana kwamba ardhi hiyo haina wenyewe. Vijana wetu pia hawawaajiri. Wakija kule wanakuja na watu wao tayari. Magari ni yao, wachimbaji ni wao, na kila kitu ni chao. Tafadhali, mutusaidie hapo. Ninaunga mkono."
}