GET /api/v0.1/hansard/entries/766993/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 766993,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/766993/?format=api",
    "text_counter": 1598,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. King’ara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": "kuhusisha wale watu ambao wako kule mashinani kama vile wale walioongea mbele yangu wamesema. Ni vizuri wale matajiri wanapotajirika, nalo eneo lile limefanya watajirike, litajirike. Lakini ukitafuta usawa wa pahali madini yametoka na pahali yanaenda kuendeleza, hakuna uhusiano kamwe. Ombi la watu wote wale wako maeneo ya madini haya ni kuwa ni vizuri wahusishwe kabla hata madini hayajaanza kuchimbwa. Tukifanya hivyo, Kenya yetu itakuwa ya kuheshimika. Itakuwa katika mrengo wa mbele wa dunia pahali madini yamekuwa ya kuleta utajiri lakini si umasikini na vita. Ninaunga mkono Hoja hii."
}