GET /api/v0.1/hansard/entries/767969/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 767969,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/767969/?format=api",
    "text_counter": 165,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Justus Murunga Makokha",
    "speaker_title": "The Member for Matungu",
    "speaker": {
        "id": 13430,
        "legal_name": "Justus Murunga Makokha",
        "slug": "justus-murunga-makokha-2"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Kwa kuwa hii ni mara yangu ya kwanza kuongea katika Jumba hili la Bunge, ningependa, kwanza, kushukuru watu wangu wa Matungu kwa kunichagua kuwa mwakilishi ama mjakazi wao katika hili Nyumba Kuu. Nikiunga mkono mapendekezo ambayo tunajadili kuhusu barabara zetu, naunga mkono Mheshimiwa mwenzangu ambaye ameongea hivi karibuni kwamba tusiongee juu ya barabara za mijini peke yake. Barabara za mashambani pia ziongezwe kwa mpangilio huu kwa sababu Kenya inakua kila siku. Barabara zetu kuu zimekuwa na shida, si ya Mombasa peke yake. Wale tunakaa sehemu hii ya upande wa Mombasa Road tuko na shida tunapokuja kazini asubuhi na tunapotoka. Pili, wale tunatoka sehemu ya Magharibi pia tuko na shida sehemu hii ya Salgaa; hutokea ajali kila mara. Tungekuwa na barabara inayoweza kutumiwa na matrela ama lori kubwa kubwa, huenda hatungekuwa na shida ambayo tunakuwa nayo kila wakati."
}