GET /api/v0.1/hansard/entries/767973/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 767973,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/767973/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Justus Murunga Makokha",
"speaker_title": "The Member for Matungu",
"speaker": {
"id": 13430,
"legal_name": "Justus Murunga Makokha",
"slug": "justus-murunga-makokha-2"
},
"content": "Nikiongezea nguvu kwa mwenzangu Mheshimiwa aliyesema ya kwamba wale wanaohusika na maneno ya sheria hawafanyi kazi yao; wamelala kwa kazi yao. Barabara mbili ambazo zilitengenezwa hivi juzi, barabara ya Eastern Bypass na Southern Bypass, zilitengenezwa kwa sababu ya kuondoa malori makubwa makubwa kupitia sehemu ya mijini. Lakini hata sasa unapotoka nje ya Bunge hili usimame utazame barabara kuu ya Uhuru Highway, utaona ya kwamba malori makubwa yangali yanatumia hii barabara. Badala ya kutumia ile barabara mpya inayopitia sehemu ya Southern Bypass, zingali zinakuja hadi mjini. Ingekuwa wale ambao wanatilia mkazo wanaona ya kwamba sheria inatumika, hatungekuwa na jambo kama hili. Ya pili, ningependa kukumbusha Waheshimiwa wenzangu ya kwamba tuko hapa kwa sababu tungependa kupeana mwelekeo. Ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba wale wanaofaa kulinda sheria na kuona ya kwamba sheria inachukua mkondo wake ndio wa kwanza kuvunja sheria. Jana ilikuwa jambo la kusikitisha kuona wale ambao wanafaa kulinda sheria wanavunja sheria. Kila Mkenya ako na haki yake. Mwenzetu Mkenya Mhe. Raila Odinga alikuwa na haki yake ya kufanya mkutano wake. Lakini lilikuwa jambo la kusikitisha jana kuona ya kwamba wale wanaofaa kulinda sheria ndio wa kwanza kuvamia Mhe. Raila. La mwisho, naunga mkono mapendekezo ya kutengeneza barabara maalum kwa ajili ya mambo yanayotokea kwa ghafla. Ahsante."
}