GET /api/v0.1/hansard/entries/768024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 768024,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/768024/?format=api",
"text_counter": 220,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Obo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nami nichangie Hoja hii. Kwanza, ningependa kumpongeza Rais wetu mpendwa kwa ukakamavu wake na busara yake aliyotumia mpaka jana tukafikia kwamba Wakenya wenyewe wanasema sasa watarudi kazini. Leo tukitoka nyumbani, tumewaona Wakenya wamejitokeza kwenda kazini. Ni kama sasa tumepata nafasi ya kufanya kazi. Tulikuwa tunashikiliwa sana. Ningependa kuunga mkono Hoja hii kwa sababu ni muhimu sana barabara za kando zitengenezwe. Utafahamu zaidi kama umewahi kuwa katika ambyulensi. Mimi nimewahi kuwa ndani ya ambyulensi na mgonjwa. Wakati upo hapo ndani na mgonjwa unatamani uweke mabawa na uruke hasa ukiona hali ya mgonjwa. Barabara hizi zitasaidia sana. Kama ilivyotajwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}