GET /api/v0.1/hansard/entries/768025/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 768025,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/768025/?format=api",
    "text_counter": 221,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Obo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "hapa, zitapunguza kupoteza uhai wa binadamu na pia zikiwekwa zitawasaidia maafisa wa polisi wa trafiki kuwashika wale wanaovunja sheria. Jana tuliwapoteza maafisa wawili wa usalama barabarani. Sababu kubwa ni kwamba barabara ni mbaya. Najua mjenzi amepewa kandarasi ya kujenga. Tunamhimiza afanye bidii maana ikiwa barabara za Lamu zitajengwa vizuri, wahalifu na wakora hawatapata nafasi rahisi kwa sababu gari zitakuwa zikienda kwa kasi. Hawatapata nafasi ya kuwaua maafisa wetu wa usalama. Natoa rambirambi kwa familia za maafisa hao wawili ambao wameuawa wakiwa kazini wakichunga usalama Lamu. Jambo lingine nataka kusema ni kwamba watu wengine wameanza kupinga ujenzi wa barabara hizi kwa sababu kwamba pengine watu wengine watakosea kwa kutofuata sheria. Wacha zijengwe. Kuna nyumba ambazo zimejengwa kwenye njia ambapo barabara zilikuwa zijengwe. Ikiwa hatua ya kisheria itachukuliwa, au kama pia zitanunuliwa, ili barabara ijengwe, ni muhimu zijengwe na sisi tuendelee kama nchi nyingine zinavyoendelea. Kule Lamu au sehemu zingine zozote, wanaojenga barabara kwa sasa pia waanze kupanga hiyo mipango ili zijengwe kama zile za kule Mpeketoni. Saa hii, hatujaanza kuwa na milolongo ya magari lakini bandari likijengwa, kutakuwa na magari mengi na sisi tusije tukawa na shida kama zile watu wa Mombasa na sehemu zingine wanapata. Nitamalizia kwa kurudi kwa Rais. Sisi watu wa Lamu tuna matumaini na imani kubwa. Nataka Rais ajue kuwa Lamu pia ni Pwani. Nimesikia wenzetu wa Mombasa na Kilifi wanalalamika kwa sababu ya marginalisation kwamba wanatengwa. Lakini sisi watu wa Lamu tunasema hata Mombasa na Kilifi wanatutenga. Lamu pia ni Pwani na sisi tumekuwa wafuasi wakubwa wa Jubilee. Tunaomba safari hii kuwe na waziri anayetoka Lamu si Mombasa na Kilifi tu. Nafasi hizo zinapewa sana watu wa Kilifi na Mombasa. Sisi pia tunao wasomi Lamu na tunaweza kuchangia waziri. Tunamuomba Rais, kwa sababu tunajua anawapenda wanyonge, anatutetea sana na kuwapenda watu wa Lamu hadi tumepata stima, aifanye ionekane katika"
}