GET /api/v0.1/hansard/entries/768042/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 768042,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/768042/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Pia, tunafurahi sana kwa sababu hatuna Kenya mbili, mbali ni hii moja. Kiti cha Rais ama Mbunge hakikaliwi na watu wawili. Ni mtu mmoja tu. Kwa hivyo, wote tunafurahi. Naambia wenzangu wote viongozi ya kwamba ni muhimu tushikane wote tuone kile kitu kitasaidia Wakenya. Ni kweli tumeona vile huyo mtoto amepigwa risasi. Kama mama na sisi kama viongozi tufikirie sana. Ukiangalia hayo mambo kwa runinga ni kama kuna watu wameanza kuvaa sare ya polisi. Ukiangalia hao polisi, unaweza kufikiria hawajapata mafunzo. Kwa hivyo, naomba Serikali iingilie kati hayo mambo ya sare za polisi kwa sababu watu wameanza kuzivaa."
}