GET /api/v0.1/hansard/entries/768043/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 768043,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/768043/?format=api",
"text_counter": 239,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Nikirudi kwa Hoja ya kutenga njia za gari za dharura, nakushuru kwa hii Hoja, kwa sababu tunafaa kuangalia kila barabara. Kwa ukweli, kuna culvert zingine ambazo zimetengenezwa kwa njia nzuri lakini kuna zile zinakaa kama milima. Hata ukiwa na mgonjwa, anaumia akirushwa kwa hizo culvert . Sisi ndio tunapitisha bajeti katika hili Bunge. Ningeomba pia tuangalie bajeti ya barabara, maji na hospitali ili tukipitisha wizara zipate pesa. Wakati mwingine pesa zinapitishwa na wizara hazipati hizo pesa. Ninatoka Samburu County ambayo ina shida kubwa sana. Mvua ikinyesha, barabara zote zinapasuka na watu hawawezi kwenda upande ule mwingine hata kwa hospitali na hawawezi kufanya chochote. Kwa hivyo, ningeomba kuwa mambo ya barabara yanafaa yaangaliwe zaidi."
}