GET /api/v0.1/hansard/entries/768045/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 768045,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/768045/?format=api",
"text_counter": 241,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Kwangu, tuna shida ya barabara. Ningependa kusema tuangalie sana katika wizara ambazo zina cartels ambazo zinapewa kazi ya kutengeneza barabara. Mtu anaweza kuchukua kampuni yake hapa, ipitishwe na apewe kazi ya kujenga barabara. Ningependekeza waanze kuzungumza na viongozi wa eneo Bunge wakati wanapeana hizo kandarasi ili wajue ni barabara gani zinatengenezwa na kwa namna gani. Unakuta kandarasi imepeanwa Nairobi na mtu anaenda Samburu na kiongozi hajui. Kwa hivyo, inafaa viongozi wahusishwe kwa yale mambo yanafanywa ndiyo tushirikiane pamoja tuone yamefanywa kwa njia inayotakikana. Unakuta vitu vingine vinaenda kombo kwa sababu viongozi hawaelezwi."
}